Kuhusu Sisi
Sisi ni shirika lisilo la faida lenye makao yake makuu nchini Tanzania linalowawezesha wanafunzi, walimu na wote wanaohitaji ujuzi muhimu wa TEHAMA ili kuungana na kila mtu KIDIJITALI.
Tumesajiliwa chini ya sheria ya NGO Tanzania kwa usajili wa namba 00NGO/R/2884

Dhamira
Kuongeza uwezo na kukuza ufahamu kupitia uhamasishaji wa rasilimali na matumizi ya teknolojia ya habari na mawasiliano kwa jamii.

Maono
Maono yetu ni kuona maarifa ya watu yakipanuliwa zaidi katika teknolojia ya habari na mawasiliano.
Tunachodhamiria kufanya
★ Kukuza matumizi ya TEHAMA katika sekta mbalimbali zikiwemo elimu na utoaji wa
elimu.
★ Kutoa elimu na matumizi ya teknolojia ya habari na mawasiliano katika shughuli za kila
siku za mtu.
★ Kukuza utoaji wa rasilimali muhimu kwa elimu ya TEHAMA kwa watu.Hii inajumuisha
utoaji wa vifaa mbali mbali kama computers, mashine za kutoa kopi, ufungaji wa
internet, projectors, maabara za kisasa(digital library) N.K
★ Kujenga ufahamu kwa watu juu ya umuhimu wa TEHAMA na kwenda sambamba na
teknolojia inayobadilika kwa kasi.
★ Kutoa msaada katika tasnia ya TEHAMA katika masuala ya vifaa na programu..
★ Kutoa mafunzo ya walimu ya TEHAMA katika elimu na kuibua uwezo wa TEHAMA
katika utoaji wa elimu.

Kwanini TEHAMA ni muhimu
Teknolojia ya habari na mawasiliano ni moja ya nguzo za maendeleo ya uchumi ambayo huleta faida ya ushindani wa kitaifa. Inaweza kuboresha ubora wa maisha ya binadamu kwa sababu inaweza kutumika kama chombo cha kujifunzia na kuelimisha, chombo cha habari, na kukuza masuala ya kiutendaji na muhimu kama vile nyanja za kiafya na kijamii. Inatoa anuwai ya maarifa ambayo inaweza kusaidia katika kupata habari.
Teknolojia ya habari na mawasiliano imekuwa sehemu ya lazima ya maisha ya kila siku ya watu wengi. Inaongeza umuhimu wake katika maisha ya watu.
Teknolojia ya kidijitali kimsingi ni juhudi ya jamii yetu kufundisha raia wa sasa na wanaochipuka maarifa na ujuzi muhimu katika vifaa vya kompyuta na mawasiliano, kudhibiti programu zao, kuendesha programu zao, na kuunda mifumo inayotumia.
Kwa hakika, tunaishi katika ulimwengu wa kidijitali unaoendelea kubadilika. TEHAMA inagusa kwa karibu kila nyanja ya maisha yetu - kutoka kazini hadi kijamii, kujifunza na kucheza. Enzi ya kidijitali imebadilisha jinsi vijana wanavyowasiliana, kujuana, kutafuta msaada, kupata taarifa na kujifunza. Ni lazima tutambue kwamba vijana sasa ni watu wa mtandaoni, wanaopatikana kupitia njia mbalimbali kama vile kompyuta, televisheni na simu za mkononi.
"Ujumbe kutoka kwa Mwenyekiti
Miaka 15 nyuma niliunda Taasisi yetu ya Mafunzo (PCTL Training Institute Limited), katika kipindi cha miaka 15 iliyopita watu wengi wasio na uwezo walitufikia wakihitaji msaada wa Mafunzo ya TEHAMA na maeneo mengine.

Kwa kutumia rasilimali kidogo tuliyo nayo; tuliwafadhili hawa wasiojiweza na kuwaweka tayari kwa kazi. Walengwa wa mpango huu wanafanya kazi katika mashirika tofauti leo na wengine wanafanya kazi katika idara tofauti hapahapa. Tuna furaha kubwa kwa hili. Kwa kupitia chuo chetu hiki tuliweza kugundua uwezo mdogo walionao watanzania wengi kwenye maswala ya TEHAMA.
Msukumo huu ulitufanya mnamo 2021 kuanza mradi mwingine wa mafunzo ya TEHAMA kwa walimu wa sekondari, tulijifunza pia mengi na majumuisho ni kwamba kwamba uhitaji wa mafunzo ya TEHAMA hauepukiki.
Tumepokea maombi mengi sana kutoka kwa shule mbalimbali wakiomba msaada katika maeneo mbalimbali kama:
– Kutoa mafunzo kwa walimu kuhusu TEHAMA
- Kuomba maabara za kompyuta
- Kuomba kompyuta mpakato kwa walimu
- Ombi la kompyuta za mezani
– Projectors
- Kuunganishwa mtandao nk
Tunafahamu nia njema ya serikali ya Tanzania ya kidijitali ( e-governance,digital schools etc) Hata hivyo ukweli ni kwamba; serikali peke yake haiwezi kufanya hivyo. Inahitaji msaada kutoka kwa watu binafsi na mashirika mbalimbali.
Hii ndio inatufanya tutamani sana kurudisha kwa wa jamii na kuisaidie serikali kufikia malengo yake.
.
.
Tunatarajia kubadilisha maisha ya watanzania kupitia NGO hii.


