Shirika lisilo la faida lililoko - Tanzania
Kuwawezesha wanafunzi, walimu na watu wote ambao wanahitaji ujuzi wa TEHAMA kufanya kazi KIDIGITALI.
TEHAMA KWA WOTE
Ilianzaje?
Wakati Powercomputers ikikamilisha miaka 20 kwa upande mmoja na kwa kuzingatia wazo la kusaidia jamii na serikali kwa upande mwingine, tuliamua kuanzisha mradi wa ICT FOR ALL - TEHAMA KWA WOTE kwenye hafla ndogo na wafanyakazi wangu.
Tumesajiliwa chini ya sheria ya NGO Tanzania kwa usajili wa namba 00NGO/R/2884
Tunatarajia kubadilisha maisha ya watanzania kupitia NGO hii..
Tunachodhamiria kufanya
Walimu waliofundishwa
Maabara za TEHAMA
Wanafunzi wa Kidato cha IV waliofunzwa
Mikutano na mikusayiko
Shule zilizotembelewa

Lengo letu ni kuongeza uwezo na kukuza uelewa wa teknolojia ya habari na mawasiliano kwa jamii ya Kitanzania.
Kwa hakika, tunaishi katika ulimwengu wa kidijitali unaoendelea kubadilika. TEHAMA inagusa kwa karibu kila nyanja ya maisha yetu - kutoka kazini hadi kijamii, kujifunza na kucheza.
Enzi ya kidijitali imebadilisha jinsi vijana wanavyowasiliana, kujuana, kutafuta msaada, kupata taarifa na kujifunza. Ni lazima tutambue kwamba vijana sasa ni watu wa mtandaoni, wanaopatikana kupitia njia mbalimbali kama vile kompyuta, televisheni na simu za mkononi.